Kimwili haupo nasi, ila tunaamini kiroho upo na sisi. Kamwe hatuwezi kuacha kukumbuka ucheshi wako. Leo haupo nasi, ila tunaamini ipo siku tutakuja kuwa pamoja tena. Tuandalie makazi mazuri huko ulipo.
Rafiki tunakukumbuka, ndugu wanakukumbuka, walimu wanakukumbuka na wote tunaokujua, tunakukumbuka.
ULALE MAHALA PEMA PEPONI KAKA MKUBWA.
DANIEL LEMA
Blog hii imeanzishwa kwa mawazo ya wanafunzi wa Mazengo Shule Msingi mwaka 2003. Huu ni mchango mmojawapo katika kuienzi shule ya Mazengo kwa yote iliyotutendea. MUNGU wetu tuongoze.
Monday, December 8, 2014
EMMANUEL MBOJE.
Kijana mcheshi na mjanja mjanja, LAKINI siyo bwege kama unavyodhani. Heshima ipo sana kama kawaida ya wanamazengo.
HESHIMA KWAKO KAKA MKUBWA.
JOEL TETTE
Kaka mkubwa ndiye mtunza muda bora kabisa kupata kutokea pale Mazengo Shule ya Msingi.
Hongera Kaka.
Hongera Kaka.
ROSE JOHN
Mjasiriamali.
Hakuna kama Mazengo hata katika nyanja hizi za ujasiriamali. Mkitaka kupata elimu ya ujasiriamali, njooni Mazengo tu. Sisi ndio namba moja.
Hakuna kama Mazengo hata katika nyanja hizi za ujasiriamali. Mkitaka kupata elimu ya ujasiriamali, njooni Mazengo tu. Sisi ndio namba moja.
EMMANUEL KAGUO
Linapokuja suala la kazi, huwa hatuna utani hatani hata kidogo. Tumezaliwa kufanya kazi, tuacheni tufanye kazi.
Asanteni sana walimu kwa muongozo wenu bora ambao leo hii unajenga maisha yetu. Mungu awazidishie.
Asanteni sana walimu kwa muongozo wenu bora ambao leo hii unajenga maisha yetu. Mungu awazidishie.
BECAUSE WE ARE HAPPY.
Tunune ili iweje? Mazengo hatuna haja ya kununa. Hata tukiwa tunashida, tunasaidiana. Sasa tumnunie nani? Kwanza hatuna papara ya maisha, pili tunafanya kazi kwa bidii, tatu tunamuomba MUNGU zaidi ya ktu chochote. Sasa ya nini tunune?
WE ARE HAPPPPPPYYYYYY.
WE ARE HAPPPPPPYYYYYY.
LINAH
Mtabaki kushangaa tu. Ndiyo hivyo, tunawanamitendo sisi. Chezea Mazengo wewe, baba la mababa Dodoma nzima.
Hongera Dada Linah.
Hongera Dada Linah.
NANI KAMA MAMA?
Jacktan Nicholous Mtewele, kadhihirisha kuwa hakuna kama Mama dunia hii. Huyu ndiye MUNGU wetu wa duniani, na ndio maana akichukia kwa sababu ya makosa uliyomtendea, inakuwa vigumu wewe kufanikiwa. Tulifundishwa hivyo Mazengo na hilo limekaa vichwani mwetu.
HONGERA JACKTAN
HONGERA JACKTAN
FRANK MASAI
Eti oooh, hawa jamaa wanajisifu tu na mambo mengine, mbona hawana wasanii?
Nani kakwambia Mazengo hamna wasanii? Utabaki hivyo hivyo. Huyo hapo msanii awezaye kupiga vifaa vyote vya muziki. Haya umeamini?
Hana shida ya kujiunga na bendi, Mazengo pekee inamtosha.
HONGERA KAKA FRANK MASAI.
TUNATAMBA KILA KONA.
Ndio hivyo jamani. Usidhani Mazengo ni wa kuja kama wale wengine. Sisi ni zaidi ya moto na vyote unavyovijua kuwa vipo juu hapa duniani. Hii ndo Mazengo bwana, ukisikia nyingine ujue kivuli, watoto wa mtaani wanakwambia hivyo.
Endelea kuwaonesha Dada yetu kuwa sisi hatuna rangi za kuunga unga, tunajiheshimu na kumuheshimu MUNGU kwa alichotupa. Hivyo ndivyo Mazengo tulivyofundishwa.
Mmmmmmmwah. (Busu kavu)
Endelea kuwaonesha Dada yetu kuwa sisi hatuna rangi za kuunga unga, tunajiheshimu na kumuheshimu MUNGU kwa alichotupa. Hivyo ndivyo Mazengo tulivyofundishwa.
Mmmmmmmwah. (Busu kavu)
MWANADADA.
Hadi nashindwa kuelezea. Huyu basi muelezeeni wenyewe, maana mimi mtaniona muongo.
Lakini nitamwelezea kidogo tu.
Mwanadada huyu bwana, hata nikisema ni mbunge au gavana, huwezi kubisha hata kidogo. Kwa sababu ana vigezo vyote vinavyokidhi sifa hizo. Mimi nampa cheo cha ugavana wa fedha. Miaka ijayo, saini kwenye noti itakaa ya huyu.
Unabisha? Kama unabisha endelea kubisha, ila mimi nimeishasema.

VENERANDA MASAI
Sisi wala hatuna shida na mtu. Uso tulivu na usio na matatizo na mtu, ndio huu hapa mnauona. Nani anabisha kuwa dada huyu ni mtakatifu? Haina ubishi hasa kwa sura yake inavyojionesha.
Mazengo hatuna tatizo bwana, ukiona tumekuletea vurugu, ujue umetuchokoza.
Mazengo Daima namba moja.
Mazengo hatuna tatizo bwana, ukiona tumekuletea vurugu, ujue umetuchokoza.
Mazengo Daima namba moja.
RAFIKI DAIMA.
Ndivyo tujuavyo. Hakuna uadui wa wenyewe kwa wenyewe wanamazengo. Bwana Rawling Richard akiwa na Hayati Nolo Ndejembi, walitudhihirishia kuwa familia ya wanamazengo ni zaidi ya ndugu. Tutaudumisha undugu daima kama hawa kaka zetu walivyouanzisha.
MAZENGO HATUDONDOKI.
UNABISHAAAAA??
MAZENGO HATUDONDOKI.
UNABISHAAAAA??
UMOJA NI NGUVU.
MAZENGO tunaamini palipo na zaidi ya wawili, basi kuna kitu kizuri kinapangwa. Naam, ndio kama hivi. Uongozi bora tuliouchagua, sasa unafanya kazi yake. Sisi ni wamoja aisee, nyie je.
TUNAKUKUMBUKA NOLLO.
Ni MUNGU pekee ajuaye mwisho wa safari yetu, leo ulikuwa nasi lakini kesho yawezekana ukawa haupo tena nasi.
Ndivyo ilivyokuwa. Tulicheka na kufurahi naye, tulikula na kunywa naye, tukacheza na kuserebuka naye, lakini leo hii haya yote yamebaki ukumbusho. Umetutoka Kaka angali bado tunahitaji tufanye mengi tukiwa na wewe.
Lakini hatutamlaumu MUNGU kwani ametoa na kutwaa, kazi yake haina makosa.
Tunazidi kukuombea MOLA akulaze mahala pema peponi.
WE MISS YOU BRO.

FERISTER KAPOSO.
Nani kakwambia Mazengo hatuwezi kutoa Miss Tanzania? Thubutuuu, kama unabisha, wekeni Miss wenu hapa nasi tumuone.
Miss Tanzania wetu huyu hapa, kama unabisha we bisha tu. Taifa limeshamchagua.
Hongera Dada yetu. Hii ndio Mazengo bwana, ukiikosa mtandaoni itafute kwenye ulimbwende. Tumetapakaa kama harufu ya shombo la samaki kule feri.
Muite Ferista Kaposo, unabishaaaaaa.
Mazengo Juuuu.

ULALE MAHALI PEMA DADA YETU.
Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa dada yetu na mdogo wetu, mwanafunzi mwenzetu na kipenzi chetu kuwa katutoka. Licha ya ugumu huo wa kutoamini, bado haikubadili ukweli kuwa Betty Ndejembi hatunaye katika maisha haya ya duniani.
MUNGU akuweke mahali salama. Wewe umetangulia, nasi tu njiani tunafuata. Njia yetu ni moja na ileile, tuandalie makazi, kwani safari yetu itaishia huko.
ULAZWE MAHALI PEMA PEPONI BETTY.
MUNGU akuweke mahali salama. Wewe umetangulia, nasi tu njiani tunafuata. Njia yetu ni moja na ileile, tuandalie makazi, kwani safari yetu itaishia huko.
ULAZWE MAHALI PEMA PEPONI BETTY.
Sunday, December 7, 2014
FARAJI KONDO.
Kaka mkubwa mwenyewe. Hakuna wa kubisha kuwa Mazengo tunawakilisha na tunatisha. Popote utakapoenda uliza kuhusu Mazengo, utapelekwa hadi kwa Waziri. Unashangaa nini? Mazengo tumetoa Mawaziri.
Huyu ni mtarajiwa.
Huyu ni mtarajiwa.
NI FURAHA TU!
Tunune kwa sababu gani sasa? Tumefundishwa maadili mema, hatuibi cha mtu, hatukabi, hatudanganyi ili tupate cha juu, hatuna mapozi, tunasaidiana. Kwa nini tusiwe na furaha?
Tacheni Wanamazengo tujiachie kwa matabasamu mwananaaaaaa.
ROMANA & RAWLING.
Tacheni Wanamazengo tujiachie kwa matabasamu mwananaaaaaa.
ROMANA & RAWLING.
NI RAHA ILIYOJE?
Hakuna kama Mazengo aiseee. Wanafunzi tusio na papara ya maisha, ni furaha tele ndiyo iliyotawala katika maisha yetu.
Pongezi zije kwako dada yetu mpendwa.
Pongezi zije kwako dada yetu mpendwa.
ERIC MTUI
Moja ya wanafunzi mahiri kupata kutokea katika shule msingi Mazengo.
Mungu akuzidishie kila pumzi ambayo ambayo unaiomba kwake.
Mungu akuzidishie kila pumzi ambayo ambayo unaiomba kwake.
EDWIN JAMES & DIANA MINJA
Jimwayeni mwayeni bwana. Hakuna anayewabugudhi, sisi ni wamoja na tutaendelea kuwa pamoja daima. Wala hatuna papara.
Mazengo Oyeeeee.
Mazengo Oyeeeee.
ALLY YASIN
Kijana mtanashati kutoka Mazengo Shule ya Msingi. Maisha ni kama raha sana kama ulipita Mazengo Shule Ya Msingi.
Shukrani ziende kwa Waalimu wote waliomfikisha kijana huyu hapa. Bila nyie asingeweza kuandika Mama wala Baba.
Heshima na Nidhamu, ninyi ndio wa kupewa pongezi.
Asanteni Walimu wote wa Mazengo.
Shukrani ziende kwa Waalimu wote waliomfikisha kijana huyu hapa. Bila nyie asingeweza kuandika Mama wala Baba.
Heshima na Nidhamu, ninyi ndio wa kupewa pongezi.
Asanteni Walimu wote wa Mazengo.
KIKAO CHA DODOMA, 2014
Wakati Dar es Salaam wanakutana, pia Mjini Dodoma baadhi ya wanafunzi wa Mazengo walikutana kwa pamoja na kujadili mambo kadha wa kadha katika kusukuma gurudumu la Muungano wa wanafamilia hii kubwa.
Hakuna Kama Mazengo Shule Ya Msingi bwanaaaaa.
Kama unabisha, hatubishani, leta hoja mezani tujadiliane kwa mifano hai. Mfano wetu huu hapa unaouona.
Hakuna Kama Mazengo Shule Ya Msingi bwanaaaaa.
Kama unabisha, hatubishani, leta hoja mezani tujadiliane kwa mifano hai. Mfano wetu huu hapa unaouona.
UKUMBUSHO.
LILIAN MSELE.
Katika ukumbusho huu wa kipekee, mwanadada huyu kaweza kuifanya Mazengo leo hii inaonekana mbele yenu.
Heshima nyingi zije kwako dada yetu.
Katika ukumbusho huu wa kipekee, mwanadada huyu kaweza kuifanya Mazengo leo hii inaonekana mbele yenu.
Heshima nyingi zije kwako dada yetu.
KIKAO CHA KWANZA CHA WANAMAZENGO DAR ES SALAAM
Ilikuwa ni furaha sana kwa nyuso hizi kukutana na kutulia kwa pamoja tena mwaka 2014 baada ya kupoteana kwa muongo mmoja.
Shukrani za dhati zimuendee MUNGU baba mwenyezi kwani katika yeye hakuna kitakachoshindikana.
MAZENGO DAIMA.
Shukrani za dhati zimuendee MUNGU baba mwenyezi kwani katika yeye hakuna kitakachoshindikana.
MAZENGO DAIMA.
Subscribe to:
Posts (Atom)