Monday, December 8, 2014

DANIEL LEMA.

Kimwili haupo nasi, ila tunaamini kiroho upo na sisi. Kamwe hatuwezi kuacha kukumbuka ucheshi wako. Leo haupo nasi, ila tunaamini ipo siku tutakuja kuwa pamoja tena. Tuandalie makazi mazuri huko ulipo.
Rafiki tunakukumbuka, ndugu wanakukumbuka, walimu wanakukumbuka na wote tunaokujua, tunakukumbuka.

ULALE MAHALA PEMA PEPONI KAKA MKUBWA.
DANIEL LEMA

JESCA

DADA yetu mpendwa. Tunazidi kukuombea, nawe tuombee kama sisi tufanyavyo.

RAHEL

Heshima zizidi kuja kwenu wanamazengo na walimu wote.

CAROLINE EDWIN

Heshima kwako dada.

EMMANUEL MBOJE.


Kijana mcheshi na mjanja mjanja, LAKINI siyo bwege kama unavyodhani. Heshima ipo sana kama kawaida ya wanamazengo.

HESHIMA KWAKO KAKA MKUBWA.

JOEL TETTE

Kaka mkubwa ndiye mtunza muda bora kabisa kupata kutokea pale Mazengo Shule ya Msingi.
Hongera Kaka.

ROSE JOHN

Mjasiriamali.
Hakuna kama Mazengo hata katika nyanja hizi za ujasiriamali. Mkitaka kupata elimu ya ujasiriamali, njooni Mazengo tu. Sisi ndio namba moja.

WALTER LUVANDA.

Hapa sisemi sana kwa sababu nikisema tu, najua kuna watu watapinga.
Kaka Mkubwa, hongera sana.

ESTER JOHN

Dada yetu mpenndwa.
Heshima nyingi zije kwako.

EMMANUEL KAGUO

Linapokuja suala la kazi, huwa hatuna utani hatani hata kidogo. Tumezaliwa kufanya kazi, tuacheni tufanye kazi.
Asanteni sana walimu kwa muongozo wenu bora ambao leo hii unajenga maisha yetu. Mungu awazidishie.

BECAUSE WE ARE HAPPY.

Tunune ili iweje? Mazengo hatuna haja ya kununa. Hata tukiwa tunashida, tunasaidiana. Sasa tumnunie nani? Kwanza hatuna papara ya maisha, pili tunafanya kazi kwa bidii, tatu tunamuomba MUNGU zaidi ya ktu chochote. Sasa ya nini tunune?
WE ARE HAPPPPPPYYYYYY.

LINAH

Mtabaki kushangaa tu. Ndiyo hivyo, tunawanamitendo sisi. Chezea Mazengo wewe, baba la mababa Dodoma nzima.

Hongera Dada Linah.

NANI KAMA MAMA?

Jacktan Nicholous Mtewele, kadhihirisha kuwa hakuna kama Mama dunia hii. Huyu ndiye MUNGU wetu wa duniani, na ndio maana akichukia kwa sababu ya makosa uliyomtendea, inakuwa vigumu wewe kufanikiwa. Tulifundishwa hivyo Mazengo na hilo limekaa vichwani mwetu.

HONGERA JACKTAN

FRANK MASAI


Eti oooh, hawa jamaa wanajisifu tu na mambo mengine, mbona hawana wasanii?
Nani kakwambia Mazengo hamna wasanii? Utabaki hivyo hivyo. Huyo hapo msanii awezaye kupiga vifaa vyote vya muziki. Haya umeamini?
Hana shida ya kujiunga na bendi, Mazengo pekee inamtosha.

HONGERA KAKA FRANK MASAI.

TUNATAMBA KILA KONA.

Ndio hivyo jamani. Usidhani Mazengo ni wa kuja kama wale wengine. Sisi ni zaidi ya moto na vyote unavyovijua kuwa vipo juu hapa duniani. Hii ndo Mazengo bwana, ukisikia nyingine ujue kivuli, watoto wa mtaani wanakwambia hivyo.

Endelea kuwaonesha Dada yetu kuwa sisi hatuna rangi za kuunga unga, tunajiheshimu na kumuheshimu MUNGU kwa alichotupa. Hivyo ndivyo Mazengo tulivyofundishwa.
Mmmmmmmwah. (Busu kavu)

MSWAKI


Kaka mkubwa unatisha sana tena sana tu.

HESHIMA KWAKO MKUU.

MWANADADA.

Hadi nashindwa kuelezea. Huyu basi muelezeeni wenyewe, maana mimi mtaniona muongo.
Lakini nitamwelezea kidogo tu.
Mwanadada huyu bwana, hata nikisema ni mbunge au gavana, huwezi kubisha hata kidogo. Kwa sababu ana vigezo vyote vinavyokidhi sifa hizo. Mimi nampa cheo cha ugavana wa fedha. Miaka ijayo, saini kwenye noti itakaa ya huyu.

Unabisha? Kama unabisha endelea kubisha, ila mimi nimeishasema.

VENERANDA MASAI

Sisi wala hatuna shida na mtu. Uso tulivu na usio na matatizo na mtu, ndio huu hapa mnauona. Nani anabisha kuwa dada huyu ni mtakatifu? Haina ubishi hasa kwa sura yake inavyojionesha.
Mazengo hatuna tatizo bwana, ukiona tumekuletea vurugu, ujue umetuchokoza.

Mazengo Daima namba moja.

RAFIKI DAIMA.

Ndivyo tujuavyo. Hakuna uadui wa wenyewe kwa wenyewe wanamazengo. Bwana Rawling Richard akiwa na Hayati Nolo Ndejembi, walitudhihirishia kuwa familia ya wanamazengo ni zaidi ya ndugu. Tutaudumisha undugu daima kama hawa kaka zetu walivyouanzisha.

MAZENGO HATUDONDOKI.
UNABISHAAAAA??

UMOJA NI NGUVU.

MAZENGO tunaamini palipo na zaidi ya wawili, basi kuna kitu kizuri kinapangwa. Naam, ndio kama hivi. Uongozi bora tuliouchagua, sasa unafanya kazi yake. Sisi ni wamoja aisee, nyie je.

TUNAKUKUMBUKA NOLLO.

Ni MUNGU pekee ajuaye mwisho wa safari yetu, leo ulikuwa nasi lakini kesho yawezekana ukawa haupo tena nasi.
Ndivyo ilivyokuwa. Tulicheka na kufurahi naye, tulikula na kunywa naye, tukacheza na kuserebuka naye, lakini leo hii haya yote yamebaki ukumbusho. Umetutoka Kaka angali bado tunahitaji tufanye mengi tukiwa na wewe.
Lakini hatutamlaumu MUNGU kwani ametoa na kutwaa, kazi yake haina makosa.
Tunazidi kukuombea MOLA akulaze mahala pema peponi.

WE MISS YOU BRO.

FERISTER KAPOSO.

Nani kakwambia Mazengo hatuwezi kutoa Miss Tanzania? Thubutuuu, kama unabisha, wekeni Miss wenu hapa nasi tumuone.
Miss Tanzania wetu huyu hapa, kama unabisha we bisha tu. Taifa limeshamchagua.

Hongera Dada yetu. Hii ndio Mazengo bwana, ukiikosa mtandaoni itafute kwenye ulimbwende. Tumetapakaa kama harufu ya shombo la samaki kule feri.

Muite Ferista Kaposo, unabishaaaaaa.
Mazengo Juuuu.

ULALE MAHALI PEMA DADA YETU.

Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa dada yetu na mdogo wetu, mwanafunzi mwenzetu na kipenzi chetu kuwa katutoka. Licha ya ugumu huo wa kutoamini, bado haikubadili ukweli kuwa Betty Ndejembi hatunaye katika maisha haya ya duniani.
MUNGU akuweke mahali salama. Wewe umetangulia, nasi tu njiani tunafuata. Njia yetu ni moja na ileile, tuandalie makazi, kwani safari yetu itaishia huko.

ULAZWE MAHALI PEMA PEPONI BETTY.