Monday, December 8, 2014

DANIEL LEMA.

Kimwili haupo nasi, ila tunaamini kiroho upo na sisi. Kamwe hatuwezi kuacha kukumbuka ucheshi wako. Leo haupo nasi, ila tunaamini ipo siku tutakuja kuwa pamoja tena. Tuandalie makazi mazuri huko ulipo.
Rafiki tunakukumbuka, ndugu wanakukumbuka, walimu wanakukumbuka na wote tunaokujua, tunakukumbuka.

ULALE MAHALA PEMA PEPONI KAKA MKUBWA.
DANIEL LEMA

JESCA

DADA yetu mpendwa. Tunazidi kukuombea, nawe tuombee kama sisi tufanyavyo.

RAHEL

Heshima zizidi kuja kwenu wanamazengo na walimu wote.

CAROLINE EDWIN

Heshima kwako dada.

EMMANUEL MBOJE.


Kijana mcheshi na mjanja mjanja, LAKINI siyo bwege kama unavyodhani. Heshima ipo sana kama kawaida ya wanamazengo.

HESHIMA KWAKO KAKA MKUBWA.

JOEL TETTE

Kaka mkubwa ndiye mtunza muda bora kabisa kupata kutokea pale Mazengo Shule ya Msingi.
Hongera Kaka.

ROSE JOHN

Mjasiriamali.
Hakuna kama Mazengo hata katika nyanja hizi za ujasiriamali. Mkitaka kupata elimu ya ujasiriamali, njooni Mazengo tu. Sisi ndio namba moja.